Back to top

UKATAJI MITI NI JANGA MIAKA MICHACHE IJAYO

28 April 2022
Share

Eneo la Misitu katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandaimba mkoani Mtwara limetajwa kupungua kwa kasi kubwa kutokana na kukithiri kwa ukataji wa miti unaosababishwa na shughuli za kibinadamu.

Kauli hiyo imetolewa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Wilaya ya Tandaimba, Mohammed Mkubagwa wakati wa upandaji wa miti zaidi ya 1000 katika shule ya msingi na sekondari Nandonde wilayani Tandaimba.

Amesema idadi kubwa ya miti imekuwa ikikatwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuchoma mkaa pamoja ukataji miti kwa ajili ya kilimo hali inayotishia uwepo wa janga katika Wilaya hiyo .

Hata hivyo ametahadharisha iwapo jamii haitachukua jitihada za makusudi kupanda miti kuna hatari miaka michache ijayo kukawa kunautegemezi mkubwa wa miti katika maeneo hayo na kusisitiza wamekuwa wakitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kulinda misitu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema miti zaidi ya elifu arobaini na moja ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda imepandwa katika wilaya hiyo na hivyo kuipongeza TFS kwa kazi kubwa wanayofanya.

Hata hivyo ametaka wakala huo kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza misitu ambayo faida yake ni kubwa kwa uhai wa binadamu huku akitaka miti yote inayopandwa kutunzwa na kulindwa ili iweze kukua na kuleta faida kwa wanachi wa eneo husika. 

Picha na Maktaba