
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof.Joyce Ndalichako amesema serikali imetangaza msamaha wa riba kwa waajiri wote waliochelewa kuwasilisha michango katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF), iliyotozwa kuanzia Oktoba 1, 2017 mpaka Agosti 31, 2021.
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam, nakueleza lengo la kufanya hivyo ni kutoa unafuu kwa waajiri na kuhamasisha kulipa michango kwa wakati kwa mujibu wa sheria.
