
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angeline Mabula amesaidia wanafunzi wenye uhitaji kwa kutoa Shilingi milioni 41.6 za masomo katika siku yake ya kuzaliwa.
"Tukiwa na utaratibu wa kuasaidia basi tutakuwa tumewasaidia wanafunzi wengi wenye uwezo wa kimasomo lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto za kifedha"Amesema Mabula.
Waziri Mabula ameitaka jamii kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi wenye uwezo wa kimasomo lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kifedha.
