Back to top

KERO ZA MUUNGANO AMBAZO HAZIJAPATIWA UFUMBUZI NI 7

20 May 2022
Share

Bunge limejulishwa kuwa hadi sasa kero za Muungano ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi ni 7 ikiwa ni pamoja na Mgawanyo wa Mapato yatokanayo na hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na faida ya Benki Kuu.

Hayo yameelezwa Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Selemani Jafo aliyetaka kujua kero  gani za Muungano ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi mpaka sasa na ni jitihada gani za makusudi zinafanyika ili kero zilizosalia  zitatuliwe.

Akaongeza kuwa mbali na kero hiyo zingine ni Usajili wa Vyombo vya Moto, Ongozeko la Gharama za Umeme kutoka TANESCO kwenda ZECO na  Malalamiko ya Wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa Kodi mara mbili.

Mhe.Jafo akaendelea kusema kuwa Kodi ya Mapato (Paye) na Kodi ya Mapato inayozuiliwa (Withholding Tax)f) Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha na Changamoto ya uingizaji wa sukari katika soko la Tanzania Bara.