Back to top

Watatu wafariki dunia katika ajali - Kahama.

24 May 2022
Share

Watu watatu wamefariki dunia hapo hapo na wengine wanne kujeruhiwa vibaya katika ajali ya Basi la kampuni ya Ruksa lenye namba  T625ARJ linalofanya safari zake kutoka Kahama Mjini kwenda Kigoma kupitia barabara ya changarawe ya Ushetu. 

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Kayenze Wilayani Kahama baada ya kumgonga muendesha baiskeli kwenye eneo la kona kali ya barabara hiyo hali iliyosababisha basi kuacha njia na kupinduka.