
Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumpata Diwani wa kata ya kawe Mutta Robert Rwakatare aliyedaiwa kutoweka tangu Februari 2022 maeneo ya Tabata Darajani akiwa kwa mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Ashura Ally Matitu (43).
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amesema baada ya Mahojiano Ashura amedai diwani huyo alifika kwake tarehe 19 mwezi huu wa tano akiwa katika mazingira ya ulevi uliopindukia na pia alidai kuwa diwani huyo ni rafiki yake wa siku nyingi kwa zaidi ya miaka 10.
Kamanda Muliro amesema wakati Jeshi la polisi likifanya uchunguzi wa kisa hicho ndugu wa diwani huyo walifika katika kituo cha polisi na wakaomba wakabidhiwe ndugu yao kwa ajili ya matibabu na tiba ya kisaikolojia.
