Back to top

Hakuna mgonjwa wa Monkeypox aliyewahi kugundulika nchini.

24 May 2022
Share

Wizara ya Afya imesema kuwa hapa nchini hakuna mgonjwa wa monkeypox aliyewahi kugundulika na imetoa rai kwa wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na kuzuia magonjwa ya kuambukiza na yale ya mlipuko ikiwa ni pamoja na usafi binafsi na usafi wa mazingira.