
Naibu Rais wa Kenya William Ruto amemwomba msamaha Rais Uhuru Kenyatta baada ya wawili hao kutofautiana pindi tu uchaguzi wa 2018 ulivyokamilika.
"Najua kuwa kuhudumu kama Naibu wa Rais huenda sikufikia matarajio ya bosi wangu Rais Kenyatta, na ninaomba unisamehe," Ruto.
Ruto ameomba msahama huo wakati wa mkutano wa kila mwaka wa maombi ya Alhamisi ulioandaliwa na bunge.
Hata hivyo Rais Kenyatta haungi mkono azma ya Ruto kuwania urais katika uchaguzi wa Agosti na badala yake anamuunga mkono kinara wa upinzani Raila Odinga.
