Back to top

USHURU KWA WAFANYABIASHA NA WABEBA MKAA KIBAHA WASHUSHWA

26 May 2022
Share


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi.Sara Msafiri ameshusha ushuru wa maliasili unaopaswa kulipiwa na wafanyabiashara na wabeba mkaa wanaotumia bodaboda maarufu (WAKUBETI ), kutoka 37,500 Hadi 30,000 ili kuondoa changamoto ya kukwepa ushuru hali iliyokuwa inasababisha kushuka kwa mapato katika Wilaya hiyo.

Ametoa kauli hiyo Kibaha Mkoani Pwani katika mkutano wa kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili wafanyabiashara wa mkaa pamoja na wabebaji kufuatia mapato kushuka kwa kiasi kikubwa hali iliyopelekea Mkuu wa wilaya hiyo kuitisha mkutano huo ili kujua changamoto zao za kukwepa ushuru wa Halmashauri.