Back to top

Membe arejea rasmi CCM apewa kadi.

29 May 2022
Share

Aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kupitia Chama cha ACT WAZALENDO Bernard Membe amerudi rasmi kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) na kukabidhiwa kadi ya Chama hicho hii leo katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Mtama, Nape Nape Nnauye uliofanyika katika Kata ya Chipomda, Jimbo la Mtama mkoani Lindi.

Akiongea kwenye tukio hili Membe amefunguka jinsi alivyoumia kutokana na uamuzi wa kumwondolea Uwanachama wa CCM na kuahidi kufia ndani ya Chama hicho ambacho amesema ndicho kilichomlea siku zote

Katika kurudi kwake CCM Membe amepokelewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka aliyekuwepo katika mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Mtama.