Back to top

MOI komesheni madaktari wasio waadilifu - Ummy

03 June 2022
Share

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Dkt.Respicious Boniface kufuatilia na kukomesha tabia ya baadhi ya Madaktari kuwaandikia wagonjwa vipimo na kuwataka kwenda kufanya katika Hospitali binafsi japokua vipimo hivyo vinapatikana hapo. 

Aidha Waziri Ummy ameonesha kusikitishwa na tabia ya baadhi ya madaktari kuwarudisha wagonjwa nyumbani bila kupata huduma japokua wamekaa muda mrefu.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara katika Taasisi hiyo kuona hali ya utoaji wa huduma za afya sambamba na kusikiliza kero za wananchi.