
Mkuu wa Kikosi Cha kuzuia wizi wa Mifugo Tanzania Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Pasua ametangaza kiama kwa watoroshaji wa mifugo nje ya nchi.
ACP Pasua amesema hayo wakati akizungumza na askari wa kikosi hicho Jijini Arusha.
Amesema zipo taarifa za watu wachache wanajihusisha na utoroshaji wa mifugo nje ya nchi, ambapo amesema kikosi hakitomuonea muhali mtu yeyote anayetorosha mifugo.
