Back to top

LISSU AELEZA MSIMAMO WAKE KUREJEA TANZANIA

07 June 2022
Share

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akiwa nchini Ubelgiji amesema hatua ya Serikali kuwataka Watanzania waliokimbia Tanzania ikiwemo yeye warejee nchini ni kauli nzuri hivyo yeye na wenzake watawasiliana na viongozi pamoja na familia zao ili kuona namna ya kurejea Tanzania.

"Hiyo ni hatua nzuri sana, kauli ya serikali imetoka sasa kitakachofanyika ni mimi na wenzangu kuanza kuandaa safari ya kurudi nyumbani, tunahitaji kuwasiliana na viongozi wenzetu walioko Tanzania, Familia zetu ili tuone tunarudije nyumbani"Amesema Lissu

Kuhusu lini na wenzake watarejea Tanzania baada ya Kauli ya serikali, Tundu Lissu hakuweza kuweka bayana tarehe rasmi ya yeye na wenzake watawaru Tanzania.

"Siwezi nikasema tarehe sasa hivi lakini angalau serikali imesema wazi kwamba tutakuwa salama, kwa hiyo sasa tunaanza taratibu za kurejea nyumbani"Amesema Lissu.

Tundu Lissu ameeleza hayo wakati akihojiwa na EATV SAA1.

Akiwa Bungeni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameeleza kauli ya serikali kwamba Watanzania wote waliokimbilia nje ya nchi kwa sababu mbalimbali kwa kuhofia usalama wa maisha yao kwa madai mbalimbali wametakiwa kurejea nchini kwa kuwa hakuna sababu yoyote ya wao kuendelea kukaa nje ya nchi kwani hali ya ulinzi na usalama kwa kila raia ni mkubwa na serikali inazingatia hilo.