Back to top

"Nyie ni mboni ya elimu hapa nchini, mnapaswa kutunzwa".Prof.Mkenda.

09 June 2022
Share

Serikali imekusudia kuimarisha ubora wa elimu nchini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa inaakisi mahitaji ya watanzania na utandawazi, na kasi ya mabadiliko ya teknolojia kwani soko la ajira limezidi kuwa pana hivyo mabadiliko yanahitajika.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf  Mkenda ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na makao makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa vijana Jijini Dodoma.

Amewataka wathibiti ubora kote nchini kusimamia kwa weledi zaidi ubora wa elimu, kwani wao ni moyo na injini ya elimu ambapo amesisitiza umuhimu wa malezi kwenye shule kwani watoto wanaanza shule mapema, huku wazazi wakiwa kwenye kinyang'anyiro cha maisha hivyo watoto wanakuwa katika mazingira ambayo hayaakisi ufanisi na nidhamu bora kwa mtoto.

"Nyie ni mboni ya elimu hapa nchini, mnapaswa kutunzwa, kuheshimiwa na kulindwa ili elimu iweze kuwa bora, hivyo pambaneni serikali imewanunuliwa magari 74 na mambo mengine chungu nzima yanakuja, msichoke".Prof.Mkenda.

Waziri Mkenda amesema kuwa Uboreshaji wa elimu kwa kupitia sera ya elimu ya mwaka 2014 na mapitio ya mitaala sio ajenda ya mtu, hiyo ni agenda ya serikali ya Tanzania.