Back to top

Dkt. Jingu awataka Wakandarasi Mji wa serikali kuongeza kasi

10 June 2022
Share

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amewataka wakandarasi wanaojenga majengo ya Wizara Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma kuongeza kasi ya ujenzi ili kumaliza kwa wakati.
.
Dkt.Jingu alitoa  kauli hiyo  Jijini Dodoma  alipofanya ziara yake kutembelea na kukagua  maendeleo ya  ujenzi  huo ambapo alisema ujenzi unaendelea vizuri  huku  akiwahimiza kuongeza wafanyakazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu (kulia) akiwa na Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe (kushoto) wakikagua Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais-Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala bora.


Aidha, Dkt.Jingu aliwaagiza kuongeza  muda wa kazi  na kuongeza vifaa  hatua itakayorahisisha kazi hiyo kufanyika kwa kasi inayotarajiwa  ili  ofisi hizo kuanza kutumika mara moja  akisema   kulingana na hali ya ujenzi baadhi ya majengo yatamalizika kabla ya muda uliopangwa.
.
“Kwa ujumla ni kwamba ujenzi unaenda vizuri  ushauri mkubwa ni tuongeze kasi ya utendaji  kazi na hasa kununua mahitaji ya vifaa kwa ujumla na wafanyakazi waongezwe itaweza kusaidia kwenda kwa kasi ambayo viongozi wetu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Mhe. Waziri MKuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine wanatarajia,” alisema Dkt. Jingu.