Back to top

JELA MWAKA 1 KWA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA GESI MKOANI MTWARA.

15 June 2022
Share

Kassim Adam Salum mkazi wa Dar es Salaam aliyeshtakiwa kwa kuharibu miundombinu ya gesi majumbani mtaa wa Kyangu katika Manispaa ya Mtwara/Mikindani mkoani Mtwara amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mtwara Lucas Jangandu.

Kwenye kesi hiyo namba 104/2021 mshatkiwa alikuwa akikabiliwa na shtaka moja la kudaiwa kuiba vifaa vya kukinga radi – EARTH RODY 5 kwenye nyumba 5 tofauti mtaa wa Kyangu tarehe 12/10/2021 huku akiwa amevaa sare kama mfanyakazi wa TPDC.

Maelezo yake ya awali mshatkiwa Kassim alipinga shtaka hilo kwa kueleza alikuja Mtwara na mwenzake, baada ya kuambiwa kuna ajira na kufikia kwenye mtaa huo wa Kyangu, lakini akajikuta akihusishwa na wizi huo huku mwenzake akifaulu kutoroka.

Hata hivyo mwendesha mashaka wa Jamhuri James Lugendo aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kuharibu miundombinu, huku mshtakiwa akijitetea, aliomba apunguziwe adhabu kwa kuwa amekaa mahabusu muda mrefu na ana familia inayomtegemea.

Aidha Hakimu Lucas Jangandu amesema ametoa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja kulingana na kanuni ya adhabu 265 na marekebisho yake ya 2016 ya mwenendo wa makosa ya jinai, huku mwanasheria wa TPDC nje ya mahakama amesema matukio kama hayo mikoa ya Lindi na Dar es Salaam yanachunguzwa.