Back to top

Watu sita wa familia moja wauawa, Kigoma.

03 July 2022
Share

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi, Menrad Singano, amesema Polisi wameanza uchunguzi wa tukio la watu sita wa familia moja wakazi wa kitongoji cha Kakonkwe kijiji cha Kiganza wilayani Kigoma kuuawa na watu wasiojulikana , usiku wa kuamkia leo, kwa kuwapiga na kitu chenye ncha kali vichwani na mwilini, na kumjeruhi mtoto wa miaka minne, na kumwacha  hai mtoto mwingine wa miezi mitatu.