
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, ametoa maelekezo kwa makamanda wa jeshi hilo waliopewa dhamana kuhakikisha wanasimamia fedha za umma na kuonesha thamani ya fedha hiyo kwa kukamilisha miradi kwa wakati ili jamii iweze kupata huduma kwa urahisi.
IGP Sirro ametoa maagizo hayo muda mfupi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kukagua mradi wa ujenzi wa upanuzi wa jengo la Hospitali ya Rufaa ya Polisi na Ujenzi wa kituo kikuu cha Polisi, daraja A cha Wilaya ya Kigamboni na kuridhishwa na kasi ujenzi wa majengo hayo.
