Back to top

Watatu wafariki, ugonjwa usiojulikana Lindi

13 July 2022
Share

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt Aifelo Sichalwe amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa usio wa kawaida kutoka katika kituo cha afya cha Mbekenyera kilichopo wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ambao hadi kufikia Julai 12, 2022 kulikuwa na wagonjwa 13 ambapo 3 kati yao wamefariki dunia.
.
Hata hivyo, Dkt. Sichalwe amebainisha kuwa Wizara iliunda timu ya wataalam kutoka idara ya Magonjwa ya Dharura na Majanga, Epidemiolojia, Mkemia Mkuu wa Serikali, NIMR, Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambao waliungana na timu ya Mkoa ikihusisha Idara ya Mifugo kwa ajili ya uchunguzi.