
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo ya makamanda wa Polisi wa mikoa mbalimbali ambapo Kamishna Msaididzi wa Polisi (ACP) Ramadhan Kingai ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni amehamishiwa mkoani Kigoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) James Manayama ambaye anastaafu.
.
Aidha, IGP Sirro amemuhamisha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mtatiro Kintikwi kwenda Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kuchukua nafasi ya Ramadhan Kingai ambaye amehamishiwa mkoani Kigoma.

