Back to top

UMILIKI WA ARDHI KWA WANAWAKE WAFIKIA 25%

17 July 2022
Share

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima amesema umiliki wa Ardhi kwa wanawake umeongezeka kutoka 9% mwaka 2014 hadi 25% kwa Mwaka 2017 huku akibainisha kuwa utekelezaji wa sheria ya ardhi ya kijiji namba 5 (1999), kifungu cha 20(1) kinachotoa nafasi kwa wanawake kumiliki ardhi ndio chanzo cha ongezeko hilo.
.
Dkt. Gwajima amesema hayo wakati akitoa salamu za serikali kwenye Kongamano la Wanawake Tanzania, lililofanyika jijini Dar es Salaam lenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake kwenye masuala ya imani na mahusiano.