
Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi SP Solomoni Mwangamilo amewaonya baadhi ya wamiliki wa mabasi na madereva yaendayo mikoani kuacha mara moja tabia ya kushabikia mwendo ambapo amesema kuwa mwendo kasi umekuwa chanzo cha kupoteza maisha ya watu.
SP Mwangamilo amesema hayo wakati akiongea na madereva wa mabasi yaendayo mikoani katika stendi kuu ya mabasi Jijini Arusha ambapo amesema kuna taarifa kutoka kwa wananchi wema kuwa kuna baadhi ya wamiliki wanao washawishi madereva kwenda mwendo kasi na madereva hao kuyaendesha magari hayo kasi kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu wa sheria za usalama Barabarani.
Mwangamilo ameongeza kuwa atakaye kamatwa kuhusika na vitendo hivyo vya uvunjifu wa sheria za usalama Barabarani hatua kali za kisheria zita chukulia dhidi yake ikiwa nipamoja na kufungiwa leseni yake kwa kipindi Cha miezi sita.
Aidha SP Mwangamilo amewahimiza madereva ifikapo Agosti 23 mwaka huu kujitokeza kuhesabiwa ili kuweka takwmu sahihi ambazo zinamanufaa kwa kila mmoja wetu.
Kwa upande wa baadhi ya madereva wamelishukuru Jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani kwa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa madereva ambayo wamesema inawajenga katika kazi yao.
