Back to top

WAZIRI DK NDUMBARO AAGIZA RITA KWENDA KIDIJITALI

27 July 2022
Share

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Dk.Damas Ndumbaro ameagiza Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kuhakikisha unasajili kidijitali watoto wote wanaozaliwa mwaka huu hasahasa wale wanaozaliwa katika mikoa ya mipakani.

Ndumbaro ametoa maagizo hayo alipotembelea ofisi za wakala huo Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma pamoja na kutembelea kituo cha afya cha Namtumbo kujionea zoezi la usajili unaofanywa kwa njia ya Kidijitali.

Kadhalika Mhe. Waziri Ndumbaro ametaka watoto wote watakaoandikishwa kuanza chekechekea au kidato cha Kwanza kuhakikisha wanakuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wiaya ya Namtumbo, Dk Julius Ningu amesema kuwa watahakikisha wanatoa elimu zaidi kwa wananchi ili waweze kujua umuhimu wa kuhakikisha watoto wanakuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Naye Mbunge wa Namtumbo, Mhe.Vita Kawawa amepongeza utaratibu huo wa kusajili na kutoa vyeti kidijitali kwani utawarahishia wananchi wengi waliokuwa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kupata vyeti vya kuzaliwa, kifo au talaka na kusema hatua hiyo itaongeza usajili zaidi.

WAZIRI NDUMBARO AAGIZA RITA KWENDA KIDIJITALI