Back to top

Tanzania mafuta bei rahisi ukilinganisha na nchi zingine EAC

27 July 2022
Share

Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba amesema Tanzania ndio nchi inayouza mafuta kwa gharama ndogo zaidi ukilinganisha na nchi zingine za Afrika Mashariki huku akibainisha kuwa bila ruzuku ya Bilioni 100 inayotolewa na Rais Samia, bei ya Mafuta ingekua imeongezeka 500 kwa kila lita ya Diesel na 200 kwa kila lita ya Petrol.
.
Mhe.Makamba ameyasema hayo akiwa ziarani katika kijiji cha cha Kilando kilichopo wilayani ya Nkasi Mkoani Rukwa, baada ya wananchi kuwasilisha kilio cha gharama ya mafuta ya Petrol na Diesel.