
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa wapya 9, amewahamisha vituo vya kazi 7, waliobakia kwenye vituo vyao 10 huku wengine wakiondolewa kwenye nafasi hizo.
.
Ambapo miongoni walioondolewa katika nafasi hizo ni:-
1. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi.
2. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila.
3. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Marco Gaguti.
4. Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Singida, Bilnith Mahenge.
5. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel.
6. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai.
