Back to top

Tanzania kunufaika na msaada wa dola bil. 30

19 August 2022
Share

Serikali ya Tanzania inatarajia kunufaika na mpango wa msaada wa miaka mitatu utakaogharimu dola za Marekani bil. 30, ulioahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping, wa kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na umasikini.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba Jijini Dar es Salaam alipofanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Qian Keming, wakati wa mkutano wa 6 wa Kamati ya Pamoja ya Uchumi, Ufundi na Biashara kati ya Tanzania na China.