Back to top

Kamanda Mutafungwa atoa maagizo kudhibiti ajali.

20 August 2022
Share

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Wilbroad Mutafungwa amewaagiza wakuu wa usalama Barabarani wa Mikoa na Wilaya kufanya doria barabarani kila siku na kuwakamata na kuwapiga faini madereva wazembe wasio weka alama za ishara (viakisi mwanga) kwenye magari yaliyoharibikia barabarani. 

Kamanda Mutafungwa ametoa agizo hilo baada ya kuzindua tamasha la kutoa elimu ya kupinga na kutokomeza ajali katika Stendi ndogo ya mabasi ya CDT Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Pia ameagiza wamiliki wa shule wote wenye magari yanayobeba wanafunzi kuyafikisha kwenye ukaguzi na kupewa vyeti maalum ambapo ameelekeza kuwa gari lolote ambalo halitakaguliwa halitaruhusiwa kubeba wanafunzi na halitatakiwa kuonekana barabarani.

Pia Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani limewaonya madereva wanaoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa huku Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Wilbroad Mutafungwa akiwataka wamiliki wa magari ya mizigo na abiria kuyasimamia magari yao kikamilifu.