
Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Dickson Mwenda mwenye umri wa miaka 37 anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 15 ndani ya gari.
.
Ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo baada Mama wa mtoto kumkabidhi mtuhumiwa mtoto huyo akiwa na mdogo wake ili awapeleke nyumbani lakini akiwa njiani aliegesha gari pembeni ya barabara kisha kutekeleza ubakaji huo ndani ya gari.
