
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), mkoani wa Morogoro, imewafikisha katika mahakama ya wilaya ya Kilosa watu 6 wakikabiliwa na makosa matatu tofauti ikiwemo kushindwa kuomba kusajiliwa kwenye Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT), kuwazuia maofisa wa mamlaka hiyo kufanya kazi yao kwa kukataa kurudisha fomu za usajili na kushindwa kuendana na matakwa ya sheria ya kodi ya ongezeko la thamani.
