
Aliyekuwa Mgombea Urais wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga amesema anataka kujua ukweli juu ya kilichojiri katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 9 nchini humo na mchakato wa kujumlisha kura huku akiwanyooshea kidole makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kutozungumza kwa sauti moja.
.
Kiongozi huyo ameyasema hayo akiwa kanisani mjini Kibra ambapo amebainisha kuwa anatafuta ukweli ili kuhakikisha kuwa kuna haki, amani na maridhiano.
