
Mahakama ya Juu nchini Kenya imeagiza masanduku ya kura ya vituo 15 yafunguliwe kwa ajili ya ukaguzi, uchunguzi na kuhesabiwa upya ambapo imeamuru zoezi hilo lifanyike ndani ya saa 48, kuanzia leo saa 2:00 usiku, Agosti 30, 2022.
.
Aidha Mahakama hiyo imebainisha kuwa wakati wa kuhesabu kura kila upande utawakilishwa na mawakala wawili na Msajili wa Mahakama ya Juu atasimamia zoezi hilo.
