
Serikali imetolea ufafanuzi wa awali kuhusu malalamiko ya wananchi yanayoendelea juu ya tozo za miamala ya simu na benki na imewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho serikali inafanyia kazi hoja hizo.
Serikali imesisitiza kuwa itaendelea na tozo hizo ambazo zimekua ni mwarobaini katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Akitoa kauli hiyo ya Serikali Jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba amesema sababu za serikali kuendelea na tozo za miamala ya simu na benki na kuwatoa hofu wananchi katika kipindi hiki, ambacho serikali inafanyia kazi malalamiko hayo.
Dakta.Mwigulu Nchemba ametolea ufafanuzi juu ya malalamiko ya kodi ya upangishaji majengo ambapo amekiri kuwa serikali inafanyia kazi malalamiko ya wananchi.
