Back to top

Naheshimu maamuzi, lakini sikubali - Raila Odinga

05 September 2022
Share

Kiongozi wa Chama cha Azimio la Umoja - ONE, Raila Odinga amesema Chama hicho kinaheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu uchaguzi wa Urais uliofanyika Agosti 09, 2022, ingawa hakikubaliani vikali na uamuzi huo, uliomthibitisha Naibu Rais, William Ruto kuwa Rais wa Mteule wa nchi hiyo. 
.
Hata hivyo, Odinga amebainisha kuwa hukumu hiyo sio mwisho wa harakati zao, lakini inawachochea kuongeza juhudi za kubadilisha nchi hiyo kuwa na demokrasia inayofaa.