Back to top

Bashungwa aagiza walimu kupelekewa huduma shuleni

08 September 2022
Share

Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kuhakikisha wanawasimamia watendaji wanaotoa huduma kwa walimu huku akiwaelekeza watendaji hao kuwafuata walimu shuleni na kutatua kero na malalamiko yao kwa wakati ambapo amepiga marufuku, kuwaacha walimu kupita kila ofisi ya Halmashauri kutafuta huduma.
.
Aidha, Waziri Bashungwa amesema Mwalimu akiandika barua kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuhitaji huduma anapaswa kujibiwa kwa maandishi ndani ya siku saba baada ya kupokelewa.