Back to top

Majibu ya Waziri kuhusu haki ya faragha kwa wafungwa.

13 September 2022
Share

Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema serikali bado haiwezi kuruhusu utaratibu wa utolewaji wa haki ya faragha kwa wafungwa na wenza wao hadi baadhi ya mifumo ya kisheria itakayokidhi uhitaji ifanyiwe kazi sambamba na utekekelezwaji wa baadhi ya taratibu kwa ajili ya jambo hilo..

Mheshimiwa Masauni amesema haki ya faragha na wenza wao si haki ya msingi kama ilivyo kwa haki nyingine muhimu kama chakula, malazi na mavazi.

Mheshimiwa Masauni amesema hayo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Bahati Ndingo juu ya ni lini serikali itaweka mfumo utakaoruhusu wafungwa kupata haki ya faragha na wenza wao.