Back to top

Muongozo wa kurudisha waliokatishwa masomo unatekelezwa.

14 September 2022
Share

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu) David Silinde, amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha muongozo wa kuwarudisha wanafunzi, waliokatishwa masomo kwa sababu mbalimbali unasimamiwa na kutekelezwa.

Mhe. Silinde amesema hayo bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali aliloulizwa na Mbunge Viti Maalum, Mhe.Zaytun Seif Swai kuhusu kauli ya serikali juu ya sintofahamu, ya utaratibu wa kuwapata Wanafunzi wanaorudishwa masomoni.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, ilitoa muongozo,  wa kuwarejesha wanafunzi waliokatishwa masomo yao kwa sababu mbalimbali ili waweze kukamilisha ndoto zao kwa kupata elimu.