Back to top

Shughuli za kisiasa, Vyama viwe na subira

15 September 2022
Share

Katika kuadhimisha siku ya Demokrasia duniani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameandika makala kuhusu siku hiyo na kubainisha kuwa vyama siasa nchini vimekuwa vikidai kuruhusiwa kuendelea kufanya kazi za kisiasa, hususan, kufanya mikutano ya hadhara na wanachama wao.
.
Hata hivyo, Rais Samia amevishauri vyama hivyo kusubili maoni na mapendekezo ya Kikosi Kazi kinachoratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya vyama vingi vya siasa, juu ya marekebisho ya Sheria na Kanuni hizo, na kwamba suala hilo litatolewa tamko siku chache zijazo