
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk Dorothy Gwajima, ameagiza kuundwa mifumo ya kuwalinda watoto na kugundua utoro wa wanafunzi mashuleni, kwa lengo la kutokomeza ukatili na unyanyasaji wakijinsia, wanaofanyiwa wanafunzi wakike kwa kuachishwa masomo na kwenda kuolewa.
Dk.Gwajima ametoa agizo hilo, baada ya kukagua miundombinu ya usafirishaji wa wanafunzi kwa njia ya mabasi mkoani Shinyanga, huku akiagiza mtuhumiwa aliyekamatwa akiwafundisha watoto vitendo viovu mkoani Geita, achunguzwe na taarifa sahihi zitolewa kwa vyombo husika na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
