Back to top

WASANII WANAOHAMASISHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KUKIONA

07 December 2022
Share

Wasanii wa Tanzania wanaotunga nyimbo zinazohamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi wameonywa na kutakiwa kuacha kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
.
Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya wakati akiongea na waandishi wa habari, mkoani Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa Mamlaka hiyo haitomuacha msanii yeyote atakaehamasisha matumizi ya dawa za kulevya kupitia nyimbo.