Back to top

MENDES NA WENZAKE MBARONI, ATUHUMIWA KUMUUA MLINZI

07 December 2022
Share

Andron Nicodemus Mendes, mwenye umri wa miaka 40, mkazi wa Salasala na wenzake, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Salum Ally (mlinzi), ambaye alipotea, na baadae mwili wake kukutwa ukiwa umetupwa katika eneo la Misugusugu, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
.
Akitoa taarifa hizo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro Jumanne, amebainisha kuwa Novemba 20, 2022 mtuhumiwa Mendes alifyatua risasi ndani ya yadi yake iliyopo Tegeta Scansanca, Kinondoni, ambapo baada ya tukio hilo zilipatikana taarifa za Salum Ally kupotea na kutojulikana alipo mpaka Disemba 02, 2022 mwili wake ulipokutwa umetupwa.