Back to top

VIJIJI ZAIDI YA 8000 VYAUNGANISHIWA UMEME

08 December 2022
Share

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imefanikiwa kuunganisha umeme kwenye vijiji zaidi ya 8,000 nchi nzima, sawa na 69.6% ikilinganishwa na 2% mwaka 2007 wakati REA inaanzishwa huku mradi wa Ifakara ukiwa umekamilika kwa 80.1%.
.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Said wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ujenzi wa mradi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Ifakara unaokwenda samabamba  na ujenzi km 82 za miundombinu ya kusambaza umeme kwenye Wilaya za Kilombero na Ulanga.