
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameridhia Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Kilimo utakaohusisha Viongozi, watu mashuhuri na wadau wapya 3,000, ambapo amebainisha kuwa mkutano huo utaendeleza uimarishaji wa mifumo ya chakula na kilimo katika vipaumbele vya Serikali, kupeana taarifa na kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya mifumo imara ya chakula.
.
Maamuzi hayo ya Rais Samia yamefuata baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe.Hailemariam Dessalegn kutangaza uamuzi huo katika Jukwaa la Mtandao wa Chakula Afrika (AGRF) nchini Marekani.

