
Shirika la Reli nchini (TRC) limeanza safari rasmi kuelekea mkoani Kigoma kwa kutumia mabehewa mapya 22 ya Meter Gauge (MGR) ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma ya usafiri wa reli nchini.
.
Kupitia Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imebainisha kuwa, safari hizo zimeanza baada ya kukamilika kwa majaribio ya awali ya umbali wa km 400, kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imeridhia mabehewa hayo kuanza kazi.

