Back to top

TEKNOLOJIA ITUMIKE KWENYE, UCHAKATAJI MAZAO YA UVUVI

21 December 2022
Share

Afisa Mtaalam wa Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji wa Viumbe Maji, Hashim Muumin amewataka wachakataji wa mazao ya uvuvi nchini kutumia fursa ya teknolojia katika shughuli zao ili kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi na kukabiliana na upotevu wa mazao hayo.
.
Muumin ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wachakataji, wavuvi na wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kupitia mradi yake ya FISH4ACP, yaliyofanyika mkoani Kigoma.