
Mussa Solomoni na Ezekia Obadia wakazi wa Mji wa Mlowo uliopo wilayani Mbozi, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani mkoani Songwe kwa tuhuma za kukutwa na katoni 19 za sukari zinazodaiwa kuwa ni feki ambazo walikuwa wanaziingiza nchini kwa njia ya magendo katika mpaka wa Tanzania na Malawi uliopo wilayani Ileje.
