Back to top

WAKWAMISHAJI UPATIKANAJI MAJI KUKIONA

04 January 2023
Share

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso, amesema hatamfumbia macho wala kumuonea haya Mkandarasi atakayeshindwa kwenda na kasi ya serikali kutatua changamoto ya uhaba wa maji, katika maeneo yenye tatizo hilo hapa nchini.

Amesema hayo mjini Morogoro wakati wa ziara yake ya kukagua na kuzindua miradi ya maji katika mkoa huo.

Ameelezea kuridhishwa kwake na utendaji kazi wa watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro- MORUWASA.

Amewataka waendelee kutoa huduma nzuri kwa wateja wao ili kunufaika na huduma hiyo.