
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amesema wameanza kuona ongezeko la uzembe, kutozingatia maadili, weledi na miongozo ya serikali kwa baadhi ya watumishi wa Afya ambapo amebainisha kuwa kwa mwaka huu hawatakuwa na msamaha kwa mtu yeyote ambaye atakwenda kinyume na miongozo hiyo na wanataka wapate wachache ili iwe mfano kwa wengine.
“Nimetoka kumwambia Mganga Mkuu wa Serikali nimeanza kuona ongezeko la uzembe, kutozingatia maadili, weledi na miongozo ya Serikali kwa baadhi ya Watumishi wa Afya, hatutomfumbia macho Mtu, tunataka tuwapate wachache tuwaoneshe mfano ili iwe mfano kwa wengine kwahiyo hii hatuwezi kukubali” Ummy Mwalimu - Waziri wa Afya
