Back to top

SERIKALI KUJENGA SHULE MPYA 184 ZA SEKONDARI

07 January 2023
Share

Serikali imesema katika mwaka wa fedha 2022/23, inatarajia kujenga shule mpya za sekondari za kata 184 ambapo kila Halmashauri itapata shule moja.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu, TAMISEMI anayesimamia Elimu, Dkt. Charles Msonde, ambapo amebainisha kuwa, shule hizo zinajengwa kupitia awamu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambao utagharimu Tsh.Mil. 600 kwa kila shule.
.
Aidha, Dkt. Msonde ameeleza kuwa ujenzi huo utaenda sambamba na ujenzi wa shule mpya 5 nyingine za wasichana za sayansi zinazopaswa kujengwa kila Mkoa.