Back to top

Rais na mawaziri wakuu kuchunguzwa Peru.

11 January 2023
Share

Mwendesha mashtaka mkuu wa Peru ameanzisha uchunguzi dhidi ya Rais Dina Boluarte na mawaziri wakuu kutokana na mapigano ya wiki kadhaa ambayo yamesababisha mauaji yenye madhara makubwa "mauaji ya halaiki".

Mapigano mapya ya Peru yamesababisha vifo vya watu wengi Siku ya Jumanne, ambapo ofisi ya mwanasheria mkuu, ilitangaza uamuzi wake wa kumchunguza Bi Boluarte, pamoja na Waziri Mkuu Alberto Otárola pamoja na mawaziri wa ulinzi na mambo ya ndani.

Rais na mawaziri wake hawajatoa maoni yao hadharani kuhusu suala hilo.