Back to top

DART yatenga Mabasi makubwa 4 kwa ajili ya wanafunzi asubuhi na jioni.

12 January 2023
Share

Wakala wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) imetenga mabasi manne makubwa asubuhi na jioni kwa ajili ya kubeba wanafunzi wa shule za msingi na secondary katika njia ya Mbezi – Kimara – Gerezani na Kivukoni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa Miundombinu wa DART Dkt. Philemon Mzee, hatua hiyo inalenga kuimarisha utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo kwani kurahisisha usafiri kunaboresha mazingira ya kujifunzia.

Wanafunzi watapanda mabasi yaliyotengwa kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi 12:20 asubuhi ambapo mabasi hayo yanapoondoka kwenye vituo vikubwa. Mabasi mawili yatapeleka wanafunzi kwa njia ya Kimara hadi Kivukoni na mengine mawili kwenda Gerezani.

Mabasi yatafanya safari za kurudi na wanafunzi jioni, kuanzia Kivukoni hadi Kimara na Gerezani hadi Kimara saa 10:30 jioni hadi saa 11:00 jioni.

#TheGuardian